Friday, July 9, 2010

Mkutano wa mawakala/ Premier Betting Vendors meeting


Katika kuelekea uzinduzi wake. Kampuni ya Premier Betting iliamua kuwakutanisha mawakala wake na kujadili maswala mbali yanayohusiana na kampuni yao.

Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es salaam ambapo ulihudhuriwa na mawakala wapatao 150, na wafanyakazi wa Kampuni.

Pamoja na shughuli mbalimbali zilizofanyika katika mkutano huo, Meneja mauzo wakampuni hiyo alichukua nafasi hiyo kutangaza Gervas Benedict kama wakala bora tangu kuanzishwa kwa kampuni.

Wakala huyo aliweza kuingizia kampuni zaidi ya sh. mil 10 na pia kujiingizia faida isiyopungua sh.laki 6. kutokana na mauzo ya tiketi na pia utoaji wa zawadi kwa shindi.

Wednesday, June 16, 2010

Virtual Horse Racing

Mbio za kusisimua, kila baada ya dakika 5
Karibu katika mchezo wa mbio za farasi, (Virtual Horse Racing)
Premier Games, inakuletea mchezo wa kusisimua utakaokupelekea hujishindia pesa nyingi.

Ni rahisi kucheza. Unaweza kuchagua aina moja kati ya tano za uchezaji.

Namna ya kucheza

1. Chagua namba ya mbio utakayotumia
Angalia kwenye uso wa Televisheni na kisha chagua namba yam bio

2. Chagua farasi wako
Kuna Win, Place na Show chagua farasi mmoja kati ya wanane (1-8).
Kwa Quinella na Exacta unatakiwa kuchagua farasi wawili.

3. Andika ubashiri wako
Chagua Win, Place, Show, Quinella na Exacta.

4. Thibitisha ubashiri wako
Andika ubashiri wako katika karatasi maalum ya kuchezea (Play slip)au unaweza
Kumtajia wakala katika kituo cha mauzo.


Aina za ubashiri

Zipo aina 5 za mchezo ambazo unaweza kubashiria.

WIN:
Bashiri farasi atakayeshinda

PLACE: Bashiri farasi atakayekuwa wa kwanza au wapili kumaliza.

SHOW: Bashiri farasi atakayekuwa wa kwanza, wapili au watatu kumaliza.

QUINELLA: Bashiri farasi wawili watakao kuwa wa mwanzo kumaliza( yani wa kwanza na wa pili ) katika mpangilio wowote

EXACTA: Bashiri farasi wawili watakao maliza mwanzo ( yani wakwanza na wapili ) kwa mpangilio


Historia ya farasi

Usisahau kuangalia matokeo ya nyuma ya farasi. Matokeo ya michezo mitano ya nyuma kwa farasi wote. Matokeo yatakuwa chini ya jina la kila farasi.

Namba ‘Odds’

‘Odds’ za michezo yote zitaonyeshwa kwenye Televisheni kabla ya mchezo husika.
Kama ubashiri wako ni sahihi, ushindi wako utahesabiwa kwa kuzidisha kiasi cha pesa ulichobashiria kwa namba (odds) ya farasi husika.

Kwa mfano

Farasi namba 4 ana odds 4.5
Kiasi ulichobashiria ni 10,000TZS kwa farasi namba 4 Kushinda.

Ikiwa farasi namba 4 atashinda, utakuwa umejishindia 45,000 TZS

(10,000TZS X 4.5)


Matokeo

Matokeo yataonyeshwa kwenye Televisheni mara baada ya kumalizika kwa kila mchezo. Matokeo ya mchezo uliopita yataonyeshwa upande wa chini wa Televisheni hiyo. Au unaweza kupeleka tiketi yako kwa wakala na kuangalia kama umeshinda ua la.


Wajibu wa uchezeshaji


Ni Premeir Bingo Entertainment Africa inawajibika katika kutoa elimu juu ya michezo hii.
Pamoja na juhudi kubwa za utoaji wa elimu juu ya michezo hii tunayoifanya, tuna imani kuwa bado watu wengi hawana uelewa juu ya uchezaji wake..

Hivyo ikiwa itakuwia vigumu katika kucheza au kama kuna mtu wako ambaye ana matatizo katika uchezaji, Tafadhali, wasiliana

Meneja wa michezo
Simu namba 0764 700711

Sports betting

Miongoni mwa products zinazotolewa na Premeir Betting Entertainment Africa ni Mchezo wa kubashiri matokeo ya mpira wa miguu 'Sports betting' na Mbio za Farasi (Virtual Horse racing)

Mchezo wa kubashiri matokeo ya mpira wa miguu

Premier Betting inakuletea mchezo wa kubashiri mechi za mpira wa miguu. Ambapo utapata nafasi ya kujionea mechi kubwa na kujishindia mamilioni ya pesa kwa kubashiri matokeo.

Soma vizuri mfumo wa timu na wachezaji , tumia maoni yako kutabiri matokeo. Kasha bashiri na upate nafasi ya kujishindia.

Kwa mfano:
Unaweza kubashiri mshindi katika dakika 90, au timu gani itashinda katika dakika 45 za kwanza au hata ni magoli mangapi yatafungwa katika mchezo husika.

Usiwe na wasiwasi kama ulikuwa hujawahi kucheza mchezo wa kubashiri kwa mpira. Soma kwa makini kipeperushi hiki na pia pata maelekezo kutoka kwa wafanyakazi wetu.

Unapofanya ubashiri, kumbuka kwamba ubashiri huo ni kwa muda ule wa kawaida tu wa mchezo wa mpira wa miguu ( dakika 90). Unaweza kujumlishwa na dakika za majeruhi ambazo huongezwa na mwamuzi.

Dakika za nyongeza au penati haziusishwi kabisa katika ubashiri.

Namna ya kucheza

Unatakiwa kubashiri matokeo ndani ya dakika 90 za mchezo husika.
Matokeo ya aina tatu yanayotarajiwa ni 1, X au 2

Bashiri “1” kwa timu mwenyeji kushinda
Bashiri” X” kwa sare
Bashiri “2” kwa timu ya ugenini

Namba zinazotolewa kwa kila timu na sare.
Kwa mfano:
Man Utd Vs Chelsea
Man Utd (2.3)
Sare (3.2)
Chelsea (2.9)

Unaweza kubashiri mechi moja (single), mechi mbili (double) mechi tatu hadi 12 (multiple)

Kadri unavyochagua namba ndogo kwa timu unayobashiri ndipo unavyojiongezea nafasi ya ushindi. Namba ya timu ikiwa kubwa maana yake uwezekano wa timu hiyo kuibuka na ushindi ni mdogo.

Namba hizi za timu hutegemea na hadhi ya timu, matokeo yake kwa sasa na mfumo wa wachezaji wake.

Namna ya kupata hesabu ya ushindi

Ikiwa utabashiri katika mechi moja, ushindi wako utahesabiwa kwa kuzidisha kiasi ulichobashiria kwa namba ya timu ‘odds’ uliyobashiri.
Kwa mfano:
Man Utd (2.3) sare Chelsea (2.9)
Bashiri kwa 10,000 TZS kwa Man United kushinda (changua 1 kwa timu mwenyeji) ikiwa itashinda utakuwa UMEJISHINDIA
10,000 kiasi cha kubashiria X 2.3 (namba ya Man.Utd )= 23,000TZS
Kwa ubashiri wa mechi zaidi ya moja, ushindi wako utahesabiwa kwa kuzidisha kiasi ulichobashiria mara namba za timu (Odds) ulizochagua. Ubashiri wako lazima utimie. Kwa mfano Ikiwa umefanya ubashiri wa timu sita halafu tano ubashiri wa tano kati ya hizo ukawa sawa na moja ukakosea,Utakuwa umepoteza nafasi yako ya ushindi.
Kwa mfano:
Man Utd (2.3) Sare (3.2) Chelsea (2.9)
Barcelona (2) Sare (3.4) Real Madrid (3.6)
AC Millan (3.2) Sare (3) Intermillan (2.1)
Ukibashiri kwa 10,000TZS kwamba Man Utd (1) Real Madrid (2) na Inter Millan (X), ikiwa matokeo yatakuwa sahihi kama ulivyobashiri. Utakuwa umeshinda.
10,000 x 2.3 (namba ‘odds’ ya Man Utd) x 3.6 namba ya (Real Madrid) x 3 (namba ‘odds’ ya sare)= 248,400TZS


Masharti na taratibu
1. Bashiri matokeo ya mechi husika ndani ya dakika 90 za mchezo. Ubashiri huo hautahusisha muda wa nyongeza ama penati. Uamuzi wa matokeo kwa michezo husika upo chini ya Premier games pekee.
2. Anayebashiri mechi zaidi ya moja atakuwa mshindi tu, endapo ubashiri wake kwa mechi hizo utakuwa sahihi kwa mechi zote. Hivyo ushindi wake utakuwa kwa kuzidisha kiasi alichobashiria kwa namba za timu husika.
3. Ikiwa mchezo utaahirishwa, utaanza kabla ya muda au kuchelewa, mchezaji atarudishiwa pesa yake aliyobashiria. Suala hili litaamuliwa na wachezashaji wa michezo ya Premier.
4. Premier Games wamepewa dhamana ya kubadilisha namba za timu inazotoa ikiwa ni pamoja na kusimamisha ubashiri wa mchezo Fulani.
5. Umri wa mchezaji ni zaidi ya miaka 18.
6. Kiasi cha chini kabisa cha kubashiria ni TZS 250 ambapo kiasi cha juu cha zawadi ni TZS 20,000,000 imepangwa kwa ubashiri mmoja. Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na wakala wa Premier Bingo Entertainment Africa au wasiliana nasi kwa simu : 0764 700 700
7. Vilevile unaweza kufika ofisini kwetu Kariakoo, mtaa wa Sukuma 8/39. Dar es salaam
Cheza kwa majukumu. Ikiwa una taarifa juu ya uchezaji uliopitiliza, tafadhali wasiliana na meneja wetu kwa simu namba 0764 700 711


Michezo mingine itakayokujia hivi karibuni

Handicap
Ubashiri wa matokeo (1,X na 2) kwa mechi zilizochaguliwa, ambapo timu dhaifu itapewa goli moja wakati wa kuanza mchezo.

Kwa mfano:

Man Utd Vs Chelsea (+1)
Ikiwa mchezo halisi utaisha kwa suluhu ya 0-0 matokeo ya handicap yatakuwa Man Utd 0-Chelsea 1.
Ikiwa mchezo halisi utaisha kwa ManUtd 1-0. Matokeo ya handicap yatakuwa 1-1 sare n.k

Dakika 45

Ubashiri wa matokeo kwa dakika 45 za mwanzo tu. Hivyo matokeo ya ubashiri huu yatakuwa ni katika hizo dakika 45 za mwanzo ukijumlisha dakika za majeruhi zitakazoongezwa na mwamuzi.

Chini/ juu ya 2.5

Ubashiri wa idadi ya magoli yatakayofungwa katika mechi moja. Bashiri chini ya 2.5 kwa magoli 0-1 au 2 jumla.
Au juu ya 2.5 kwa magoli 3,4,5 au magoli zaidi.

Tuesday, June 15, 2010

Premier Bingo

Ni mchezo wa kila siku unaochezwa kwa kutumia tiketi zinazouzwa kwa bei ya Tsh. 1000 na 500 kwa nusu yake.
Tiketi hii ina namba 90, ambazo hazipo kwenye mpangilio. Namba hizo zimepangwa katika mafungu sita ambapo kila fungu lina mistari mitatu ambapo kila mstari una namba tano.
Zawadi itatolewa kwa mshdindi atafanikiwa kukamilisha mstari wa namba.



1. Atakayekuwa wa kwanza kukamilisha mstari wa kwanza atajishindia -Tsh.50,000.
2. Atakayekamilisha mstari wa kwanza katika namba 28 za kwanza atajishindia-Tsh 5,000
3. Atakayekuwa wa kwanza kukamilisha mistari miwili ya kwanza atajishindia Tsh.
200,000
4.Atakayekamilisha mistari miwili katika namba 39 za mwanzo, atajishindia Tsh.50,000

5. FULL HOUSE
Atakayekamilisha mistari mitatu katika chumba kimoja atajishindia -asilimia 8 ya
mauzo ya siku hiyo. Ikiwa mshindi ni zaidi ya mmoja watagawana kiasi kisichopungua
Tsh 250,000
6. SNOWBALL
Atakayekamilisha mistari mitatu katika namba 40 za kwanza atajishindia asilimia 10, ikiwa mshindi ni zaidi ya mmoja watagawana kiasi kisichopungua Tsh. 300,000
Ikiwa kama hakuna mshindi zawadi itaingizwa katika droo ya siku inayofuata.

Easy Bingo

Easy Bingo ni mchezo wa kila siku wa kubashiri namba kupitia tiketi zinazotolewa na mashine za Premier Betting.

Easy 1. Kubashiri namba moja katika namba tano za mwanzo katika droo, 1:10
Ikiwa utabashiria kiasi cha sh.800 una nafasi ya kujishindia Tsh.8,000.
Easy 2. Kubashiri namba mbili katika namba tano za mwanzo katika droo, 1:200.
Ikiwa utabashiria kiasi cha sh. 800 una nafasi ya kujishindia 160,000.
Easy 3. Kubashiri namba tatu katika namba tano za mwanzo kutoka katika droo,1:2,000
Ikiwa utabashiria kiasi cha 800 una nafasi ya kujishindia 1,600,000.
Easy 4. Kubashiri namba nne, katika namba tano za mwanzo katika droo 1:5000
Ikiwa utabashiria kiasi cha sh.800 una nafasi ya kujishindia Tsh 4,000,000
Easy 5.Kubashiri namba tano za mwanzo kutoka katika droo 1:50,000
Ikiwa utabashiria kiasi cha sh.800, utajishindia 40,000,000.

Droo za Premeir Betting

Droo za Premier Betting zitakazotoa namba za ushindi, zitakuwa zikifanyika kila siku saa kumi na mbili jioni. Katika Premeir Games Center, mtaa wa Sukuma karibu kabisa na Soko Kuu la Kariakoo.

Taarifa za ushindi
Taarifa za ushindi unaweza kuzipata kwa kila wakala wa Premier Betting. Au unaweza kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0764 700777. (Andika bingo kisha tarehe na mwezi uliocheza kwa mfano Bingo 0303#)

Malipo ya zawadi
Unaweza kupata zawadi yako kutoka kwa wakala yeyote aliyeishinishwa au fika katika ofisi za Premier Betting zilizopo katika Mtaa wa Sukuma katibu kabisa na Soko la Kariakoo jijini Dar es salaam.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na wakala wa PREMIER BETTING au Entertainment Africa LTD
PO BOX 15127
Kariakoo, Dar es salaam
Simu: 0764 700700
Fax: 022 2182121

Mashine ya droo za Premier Betting


Katika michezo yetu ya Premier na easy na rapid bingo droo hufanyika kila siku saa kumi na mbili kamili jioni katika ofisi zetu zilizopo mtaa wa Sukuma, karibu kabisa na soko kuu la Kariakoo.

Je unafahamu kuwa tuna mashine ya kisasa kabisa inayotumika katika droo zetu?
Ndio, Mashine hii inafahamika kama Venus
Ni mashine ya kisasa kabisa, yenye uwezo wa kuchanganya na kuchagua namba za mipira maalum ya kuchezea bahati nasibu za Premier betting.
Venus imetengenezwa kwa kutumia Teknolojia ya hali ya juu sana,ina kipenyo cha mm 500.Imetengenezwa kwa kioo hivyo ina uwezo mkubwa wa kuonyesha namna inavyofanya kazi. Umbo lake hilo huchangia kwa kiasi kikubwa mipira iliyo ndani yake kuonekana kwa urahisi na hadhira wakati wa kucheza.
Kwa kawaida mashine hii ina uwezo wa kuchanganya mipira 90 kwa wakati mmoja.Mashine hii hutumia umeme, pia ina uwezo mkubwa wa kutambua mpira feki endapo utatumbukizwa ndani yake.
Sifa zote hizi huchangia kuifanya mashine hii kufanya kazi kwa usalama uwazi na uhakika.

Premier Bingo balls
Je ungependa kujua sifa ya mipira inayotumika katika mashine hii?
Mipira hii ina kiwango cha juu cha usalama, ni myepesi na ina 'cover'maalum ambayo hairuhusu maji kupita. Si hivyo tu kutokana na namna ilivyo tengenezwa inakuwa ni vigumu kupenyeza kitu ndani yake.
Ukiachilia mbali kiwango cha ubora cha mipira hii,ina vipimo vilivyohakikiwa kwa umakini.

Mipira hii ina 3.8g
Kipenyo 44mm

michezo ya Premier Betting

Premier betting Entertainment Africa limited, ni kampuni inayojihusisha na michezo mbalimbali ya kubahatisha.

Michezo hiyo ni Easy Bingo, Premier Bingo,Rapid Bingo na sports betting.
Kupitia kurasa hizi utaweza kujipatia taarifa mbalimbali zinazohusu michezo hii pia utapata wasaa wakujionea orodha ya washindi wetu wa kila droo.

Kwa kuwa tuna ukaribu mkubwa na michezo mbalimbali utapata nafasi ya kujionea michezo ya mpira wa miguu hususani kombe la dunia pamoja na taarifa zake.