Tuesday, June 15, 2010

Mashine ya droo za Premier Betting


Katika michezo yetu ya Premier na easy na rapid bingo droo hufanyika kila siku saa kumi na mbili kamili jioni katika ofisi zetu zilizopo mtaa wa Sukuma, karibu kabisa na soko kuu la Kariakoo.

Je unafahamu kuwa tuna mashine ya kisasa kabisa inayotumika katika droo zetu?
Ndio, Mashine hii inafahamika kama Venus
Ni mashine ya kisasa kabisa, yenye uwezo wa kuchanganya na kuchagua namba za mipira maalum ya kuchezea bahati nasibu za Premier betting.
Venus imetengenezwa kwa kutumia Teknolojia ya hali ya juu sana,ina kipenyo cha mm 500.Imetengenezwa kwa kioo hivyo ina uwezo mkubwa wa kuonyesha namna inavyofanya kazi. Umbo lake hilo huchangia kwa kiasi kikubwa mipira iliyo ndani yake kuonekana kwa urahisi na hadhira wakati wa kucheza.
Kwa kawaida mashine hii ina uwezo wa kuchanganya mipira 90 kwa wakati mmoja.Mashine hii hutumia umeme, pia ina uwezo mkubwa wa kutambua mpira feki endapo utatumbukizwa ndani yake.
Sifa zote hizi huchangia kuifanya mashine hii kufanya kazi kwa usalama uwazi na uhakika.

Premier Bingo balls
Je ungependa kujua sifa ya mipira inayotumika katika mashine hii?
Mipira hii ina kiwango cha juu cha usalama, ni myepesi na ina 'cover'maalum ambayo hairuhusu maji kupita. Si hivyo tu kutokana na namna ilivyo tengenezwa inakuwa ni vigumu kupenyeza kitu ndani yake.
Ukiachilia mbali kiwango cha ubora cha mipira hii,ina vipimo vilivyohakikiwa kwa umakini.

Mipira hii ina 3.8g
Kipenyo 44mm

No comments:

Post a Comment