Tuesday, June 15, 2010

Premier Bingo

Ni mchezo wa kila siku unaochezwa kwa kutumia tiketi zinazouzwa kwa bei ya Tsh. 1000 na 500 kwa nusu yake.
Tiketi hii ina namba 90, ambazo hazipo kwenye mpangilio. Namba hizo zimepangwa katika mafungu sita ambapo kila fungu lina mistari mitatu ambapo kila mstari una namba tano.
Zawadi itatolewa kwa mshdindi atafanikiwa kukamilisha mstari wa namba.



1. Atakayekuwa wa kwanza kukamilisha mstari wa kwanza atajishindia -Tsh.50,000.
2. Atakayekamilisha mstari wa kwanza katika namba 28 za kwanza atajishindia-Tsh 5,000
3. Atakayekuwa wa kwanza kukamilisha mistari miwili ya kwanza atajishindia Tsh.
200,000
4.Atakayekamilisha mistari miwili katika namba 39 za mwanzo, atajishindia Tsh.50,000

5. FULL HOUSE
Atakayekamilisha mistari mitatu katika chumba kimoja atajishindia -asilimia 8 ya
mauzo ya siku hiyo. Ikiwa mshindi ni zaidi ya mmoja watagawana kiasi kisichopungua
Tsh 250,000
6. SNOWBALL
Atakayekamilisha mistari mitatu katika namba 40 za kwanza atajishindia asilimia 10, ikiwa mshindi ni zaidi ya mmoja watagawana kiasi kisichopungua Tsh. 300,000
Ikiwa kama hakuna mshindi zawadi itaingizwa katika droo ya siku inayofuata.

No comments:

Post a Comment